KOCHA Mfaransa wa Simba, Pierre Lechantre amewapumzisha wachezaji wake kwa takribani saa tano ili kuhakikisha wanakuwa vizuri kabla ya kuanza maandalizi ya mwisho.
Simba iko mjini hapa tayari kuivaa Al Masry katika mechi ya pili ya Kombe la Shirikisho Afrika baada ya sare ya 2-2 jijini Dar es Salaam.

Mara baada ya kusafiri kwa zaidi ya saa nane kutoka Dar es Salaam kupitia Addis Ababa, Ethiopia halafu Cairo, Misri na baadaye hapa, Lechantre aliamua kuwapumzisha wachezaji hao.

Kwanza walifikia kupata kifungua kinywa na baada ya hapo wakaanza mapumz i k o kabla ya kuanza maandalizi rasmi jana usiku.
Wacheza j i hao wameanza maandalizi ya mwisho jana usiku baada ya Mfaransa huyo kutaka wajifue usiku.
Wakati mechi inatarajia kuanza saa moja usiku, yeye alitaka wachezaji wake kuanza mazoezi mapema zaidi.
Simba imeanza kufanya mazoezi jioni ili kuhakikisha inazoea mazingira na hali ya hewa kabla ya kuwavaa Al Masry.