
Kikosi cha Simba Sc ya jijini Dar na viongozi wa timu hiyo, jana walipata fursa ya kukutana na Balozi wa Tanzania nchini Misri, Issa Nassor, nyumbani kwake nchini humo na kufanya mazungumzo mafupi.

Simba walialikwa na Balozi huyo baada ya mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Al Masry kumalizika ambapo walitoka sare ya bila kufungana.

Baada ya mwaliko huo kutoka kwa Balozi Nassor, Simba hivi sasa wako njiani kurejea nyumbani, jijini Dar es Salaam baada ya kuondolewa katika michuano hiyo ya kimataifa ya kombe la shirikisho barani Afrika.