Kipindi cha Spoti Hausi leo kitachambua mambo mengi kuhusiana na soka la Tanzania lakini kubwa kabisa ni ushauri kama kweli Donald Ngoma alikuwa anaumwa kipindi chote alichokuwa nje au alitaka kuona kama Yanga itafika mbali kwenye michuano ya kimataifa na ligi ndiyo arudi.
Lakini pia ni uchambuzi wa mchezo wa Kombe la FA kati ya Yanga na Singida, huku timu hiyo ya Singida ikiwa na changamoto ya kukosa wachezaji wake wengi ambao wameikimbia kutokana na matatizo ya kimkataba.
Pia, mshindi wa Shindano la #BeatsByDre kutoka Gazeti la #SpotiXtra linalotoka kila Jumapiliatatangazwa leo kupitia droo maalum itakayochezeshwa kwenye Kipindi cha #SpotiHausi SAA 10:00jioni kupitia #GlobalTVOnline.
Washindi wengine watakaotangazwa ni wawili ambao watajinyakulia jezi za vilabu vya Ligi Kuu ya England.
