×

CAG Aomba Radhi Kuhusu Deni la Taifa -Video

MDHIBITI na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, Musa Assad Ameomba radhi kwa usumbufu ulijitokeza baada ya kutoa taarifa za ripoti yake aliyoikabidhi kwa Rais John Magufuli hivi aribuni, Ikulu jijini Dar es Salaam.

 

Katika ripoti hiyo ambayo kisheria ilitakiwa kupelekwa Bungeni kujadiliwa na baadae kuwekwa wazi kwa wananchi, kuhusu deni la taifa CAG amesema kuwa deni la taifa linavumilika tofauti na hapo awali kawa halivumiliki.

 

Siku ya kukabidhi ripoti hiyo, Assad alisema deni lataifa limeongezeka kutoka Shilingi trilioni 41 hadi Shilingi trilioni 46 kwa mwaka 2017/2018.

VIDEO: MSIKIE HAPA AKIFUNGUKA.