
- Mshindi wa Sh. milioni 260 wa Tatu Mzuka, James Msengi (kulia), akipokea hundi yake kutoka kwa Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Tatu Mzuka, Sebastian Maganga,(katikati). Kushoto ni ofisa kutoka bodi ya michezo ya kubashiri, Baka Maggid, akishuhudia makabidhiano hayo.

- …Akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Rufiji (katikati), Juma Abdallah Njayo, ofisini kwake Rufiji na wafanyakazi wenzake.

- …Akiwa kwenye pozi na mkewe, Neema Msengi.

- Baadhi ya waandishi wa habari wakishuhudia makabidhiano ya hundi kwa mshindi huyo.

- …Akiwa ameketi nyumbani kwake Ikwiriri na mkewe Neema.
KAMPUNI ya michezo ya kubashiri ya Tatu Mzuka, mapema leo imemkabidhi kitita cha shilingi milioni 260, Ofisa Kilimo na Ufugaji wa Rufiji Mwalimu James Msengi ambazo alishinda kwenye droo iliyochezeshwa usiku wa Jumapili iliyopita.
Hundi hiyo amekabidhiwa mapema leo na Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Tatu Mzuka, Sebastian Maganga, huku akishuhudiwa na ofisa kutoka bodi ya michezo ya kubashiri, Bakari Maggid, ndani ya ukumbi wa Hoteli ya Lamada Posta jijini Dar es Salaam.
(Stori na Picha: Musa Mateja | Global Publishers