×

ROBERTO CARLOS; BEKI MSHAMBULIZI MWENYE JINA KUBWA UEFA

ROBERTO Carlos ni mmoja wa wache­zaji wenye historia kubwa katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya. Kwanza, ame­beba taji hilo mara tatu, pia aliwahi kufanikiwa kuwa beki bora wa klabuza Uefa al ipofanya maajabu kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa mwaka 2002 na 2003.

 

Carlos, aliyezaliwa Aprili Mosi, 1973, ni Mbrazili ambaye jina lake kamili ni Roberto Carlos da Silva Rocha. Alianza maisha yake ya soka akiwa fowadi lakini baadaye alibadi­li namba, na maisha yake karibu yote ya soka alicheza kama beki wa kushoto.

Carlos, 44, ame­kuwa akitajwa kuwa katika historia ya soka, ni beki namba moja wa kushoto ambaye akili yake inawaza kushambulia zaidi.

 

Carlos alipewa jina la utani la “The Bullet Man” kutokana na kuwa na miguu yenye nguvu, iliyopiga mipira ya faulo kwa ustadi mkubwa, faulo zake zilipimwa kuwa zilikuwa na uwezo wa kwenda kilometa 169 kwa saa.

Gwiji huyu alijulikana kwa stamina, kasi ya kukimbia, uwezo wa kupiga kro­si, kurusha mipira mirefu, na paja lake li­likuwa na uku­bwa wa inchi 24 au sentimita 61.

 

Mwaka 1997, licha ya kuwa beki, Carlos alifanikiwa kuwa mchezaji bora namba mbili wa dunia. Huyu ni mmoja wa mabeki bora zaidi wa kushoto wal iowahi kutokea ka­tika soka. Alipata umaarufu mkubwa akiwa na kikosi cha Real Ma­drid.

Katika ngazi ya kimataifa , Carlos ali­cheza kwenye michuano mitatu ya Kombe la Dunia, akaisaidia Brazil kufika fain­ali mwaka 1998 nchini Ufaransa, na kushinda taji hilo mwaka 2002 Ko­rea/Japan.

 

Car­los aliichezea Real Madrid kwa mis­imu 11 ya mafani­kio. Klabuni hapo, alishinda mataji manne ya La Liga, na matatu ya Ligi ya Mab­ingwa Ulaya. Aprili 2013, alita­jwa na Gazeti la Marca la nchini Hispania , kuwa mmoja wa “Kikosi cha Wachezaji 11 Bora wa Kigeni katika His­toria ya Real Madrid.”

 

Pale Madrid, ali­pewa sifa ya kwamba akiwa upande wa kushoto anaweza kucheza mwenyewe namba tatu na 11, kwa maana ya ku­kaba na kushambulia. Kocha wa zamani wa Real Madrid, Vicente del Bosque, aliwahi kusema: “Ana uwezo mkubwa wa kulinda na kushambulia mwenyewe eneo lote la kushoto.”

Carlos, alikuwa beki wa kushoto wa kutu­mainiwa wa Real Madrid kwa mis­imu kumi mfu­lulizo kuanzia 1996-97 hadi 2006-07. N d i y e mc h e ­zaji ali­yeza­liwa nje y a H i s ­pania, ali­yeichezea Madrid mechi nyingi zaidi za La Liga kihistoria (370).

Enzi zake, Carlos alikuwa sambamba na gwiji wa AC Milan, Paolo Maldini, wakitajwa kuwa ma­beki bora zaidi wa kushoto dun­iani.

 

Katika fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya mwaka 2002, Carlos anakum­bukwa kwa kutoa pasi safi ya bao kwa Zinedine Zidane ambaye alifun­ga bao linalojulikana kama bao bora zaidi kufungwa katika historia ya mi­chuano hiyo.

Ukiachana na ishu ya kutajwa kuwa beki bora wa Uefa 2002 na 2003, pia alijumuishwa katika timu bora ya Uefa miaka hiyo. Carlos pia al­isifika kwa k u ­funga mabao makali.

 

Mbrazili mwenzake, Ronaldinho aliwahi kusema kwamba Carlos alikuwa muhimu katika kila ubingwa wa Ligi ya Mab­ingwa ambao Madrid iliupata ak­iwemo.

Siku ya mwisho ya msimu wa 2002-03, wakati Real Madrid ikitak­iwa kuichapa Athletic Bilbao ili kut­waa ubingwa wao wa 29 wa La Liga, Carlos alifunga bonge la bao kwa faulo na kufanya matokeo kuwa 2-1, mwisho Madrid ilishinda 3-1 na kut­waa ubingwa.

 

Desemba 6, 2003, Carlos alifun­ga bao la kwanza walipoichapa Barcelona katika Uwanja wa Camp Nou, huo ulikuwa ush­indi wa kwanza wa Real Madrid kwenye uwanja huo katika kipin­di cha miaka 20.

Bao lake la mwisho Real Ma­drid lilikuwa la ushindi katika dakika za nyongeza dhidi ya Rec­reativo de Huelva msimu wa 2006–07. Bao hilo liliisaidia Ma­drid kubeba ubingwa wake wa 30 wa La Liga, ambapo walikuwa sawa kwa pointi na Barcelona la­kini wakawa mabingwa kwa faida ya uwiano mzuri walipokutana ‘head to head’.

 

Carlos alistaafu soka rasmi Agosti 2012, akiwa na umri wa miaka 39. Alirejea dimbani katika kikosi cha Delhi Dynamos lakini alicheza mechi tatu tu.

MATAJI

Palmeiras:

Ligi Kuu ya Brazil (Campeonato Brasileiro Série A (2): 1993, 1994

Campeonato Paulista (2): 1993, 1994

Torneio Rio-São Paulo: 1993

REAL MADRID:

La Liga (4): 1996–97, 2000–01, 2002–03, 2006–07

Supercopa de España (3): 1997, 2001, 2003

Ligi ya Mabingwa Ulaya (3): 1997– 98, 1999–2000, 2001–02

Intercontinental Cup (2): 1998, 2002

Uefa Super Cup: 2002

FENERBAHÇE:

Turkish Super Cup (2): 2007, 2009

BRAZIL:

Kombe la Dunia: 2002

Copa América (2): 1997, 1999

Kombe la Mabara: 1997

MAISHA BINAFSI

Roberto Carlos amemuoa mwa­namke mrembo wa Kibrazili, Mari­ana Luccon tangu 2009. Ana watoto nane, wa kiume wanne na wa kike wanne.

ANACHOKIFANYA KWA SASA

Baada ya kus­taafu soka, Carlos alianza ukocha. Alikuwa kocha wa Sivass­por katika Ligi Kuu ya Uturuki kuanzia 2013, alijiuzulu Desem­ba 2014. Kuanzia Julai 2015, ni kocha wa Delhi Dynamos.

 

GOLI la Okwi Lililoipatia Simba Ushindi, Simba 1- 0 Mtibwa Sugar