
HAKIKA ni simanzi, vilio na majonzi baada ya wasanii kuwasili nyumbani kwao marehemu Agness Gerald Masongange na kuliona kaburi mabamo aanatarajiwa kuzikwa staa huyo katika Kijiji cha Utengule, Mbalizi Mbeya.

Mwili wa marehemu umewasili kijijini hapo mapema leo baada ya jana kuagwa katika viwanja vya Leaders jijini Dar es Salaam.

Masogange alifariki dunia Ijumaa iliyopita katika kituo cha Huduma za Afya cha Mama Ngomakilichopo Mwenge jijini Dar ambapo jana aliagwa katika Viwanja vya Leaders na kusafirishwa kwenda kwao kuzikwa.









PICHA NA HILALLY DAUDI | GLOBAL TV ONLINE, UTENGULE, MBALIZI, MBEYA