
Mchezo wa kiwango cha kipekee wa Mohamed Salah uliisaidia Liverpool kuchukua ushindi wa nguvu wa nusu fainali ya Kombe la Vilabu Bingwa Ulaya licha ya mabao 2 ya dakika za lala salama ya Roma.

Liverpool ambao pia walifanikiwa kufika fainali ya 2007, waliipita safu ya ulinzi ya Roma bila pingamizi na kufunga mabao matano katika dakika 68 za kipindi cha kwanza na cha pili katika Uwanja wa Anfield.

Salah ambaye kwa sasa amefunga mabao 43 tangu ahamie Liverpool kutoka Roma alifunga mabao mawili na kutoa assists mbili.

Bao la kwanza na la pili alifunga Salaha huku bao la tatu akimpatia pasi murua adio Mane kufanya mambo kuwa 3-0, kabla ya kutoa pasi nyingine kama hiyo kwa mshambuliaji Robert Firminio aliyefunga bao la nne.

Liverpool ilikuwa timu ya pili kufunga mabao matano katika mechi ya nusu fainali ya kombe la Vilabu bingwa Ulaya wakati Firmino alipofunga kwa kichwa kona iliopigwa na James Milner.

Huku timu yake ikiongoza 5-0 baada ya dakika 68, Mkufunzi wa Liverpool Jurgen Klopp alimuondoa Salah na Roma ikajipatia fursa katika mechi ya marudio wiki ijayo katika Uwanja wa Stadio Olimpico.

Kwanza Eden Dzeko aliifungia timu yake bao la kwanza kutoka kwa pasi ya Radja Nainggolan na baadaye Diego Perotti alifunga mkwaju wa penalti baada ya Milner kuunawa mpira katika eneo hatari.

Sasa Roma itahitaji kutumia kila mbinu ili kushinda 3-0 nyumbani Italy ili kusonga katika fainali ya kombe hilo.

Wiki mbili zilizopita Roma iliwashangaza mabingwa wa Uhispania Barcelona kwa kuwalaza 3-0 baada ya Barcelona kuicharaza timu hiyo 4-1 katika duru ya kwanza.

Iwapo watafanikiwa kuilaza Liverpool nyumbani basi wataingia katika fainali dhidi ya Bayern Munich ama Real Madrid ambao wanakutana leo Jumatano kwa mechi nyengine ya nusu fainali.

Mbali na mabao mawili yaliofungwa na Roma katika kipindi cha pili cha mechi kiungo wa kati wa Liverpool Alex Oxlaide-Chamberlain alitolewa uwanjani kwa machela baada ya kupata jereha.
Kocha Jurgen Klopp anasema kuwa huenda kiungo huyo alipata jeraha ‘baya sana’.

LIVERPOOL: Karius 6, Alexander-Arnold 6.5, Lovren 7, Van Dijk 7, Robertson 7, Oxlade-Chamberlain 6 (Wijnaldum 17 6.5), Henderson 6.5, Milner 7, Salah 9 (Ings 74 6), Firmino 8.5 (Klavan 90), Mane 7
Goals: Salah 36, 45, Mane 56, Firmino 62, 69
Bookings: Alexander-Arnold, Lovren
SUBS NOT USED: Mignolet, Clyne, Moreno, Solanke
Manager: Jurgen Klopp 8
ROMA: Alisson 6, Fazio 4.5, Manolas 6, Juan Jesus 5.5 (Perotti 67), Florenzi 6, De Rossi 6 (Gonalons 74), Strootman 4.5, Kolarov 5, Under 4.5 (Schick 45), Nainggolan 5, Dzeko 6
Goals: Dzeko 81, Perotti pen 84
Bookings: Juan Jesus
SUBS NOT USED: Skorupski, Lorenzo Pellegrini, Bruno Peres, El Shaarawy.