
MKONGWE wa filamu kutoka Nollywood, Chika Ike ameamua kuachana ‘kupiga chini’ kuigiza na kujikita rasmi kwenye biashara.
Chika ambaye ana shahada ya biashara katika Chuo cha Biashara cha Harvad, Boston nchini Marekani, alisema hajaingia darasani kusoma kwa kujifurahisha.“Sitaki kuigiza tena, nafanya biashara.”
Hivi karibuni, staa wa filamu Nigeria, Uche Maduagwu aliweka hadharani kuwa angependa kumuoa Chika kwa sababu ni mwanamke mchapakazi. Chika amewahi kutamba na filamu kibao zikiwemo Dangerous Beauty, The Missing King, Battle Man, Breathe of Love, Road to Hell pamoja na To Love a Stranger.
LAGOS, Nigeria