×

Breaking News: Magari Yaliyobeba Polisi, Wanajeshi Yapata Ajali Moro

Polisi na wanajeshi wakiendelea kutoa gari baada ya kutokea kwa ajali eneo la Bwawani.

Basi lililokuwa limebeba askari Polisi limegongana na gari dogo aina ya Noah iliyokuwa imebeba Wanajeshi wa JWTZ, katika maeneo ya Bwawani mkoani Morogoro.

Imeelezwa kuwa basi hilo la Polisi lilikuwa likitokea jijini Dodoma kwenye sherehe za Muungano zilizofanyika jana Aprili 26, 2018 huku Noah hiyo iliyokuwa na Wanajeshi takribani 6 pamoja na mtoto ikitokea Morogoro. Majeruhi wote wamepelekwa hospitali Morogoro

Hata hivyo, bado hakuna taarifa rasmi lakini habari za awali zinasema askari wawili wamefariki papohapo ingawa  Kamanda wa Polisi, Ulrich Matei amesema atatoa taarifa za kina baaadae.