
MKALI wa Bongo Fleva, Esterlina Sanga ‘Ndege Mnana’ au Linah, amesema anamshukuru Mungu kwa kumjalia
kupata mtoto kwa sababu kuna watu wengi wametamani kuwa mama lakini imeshindikana.
Akizungumza na Over Ze Weekend, Linah alisema kuwa hapendelei kukaa mbali na mwanaye huyo wa kike aitwaye Trecy kwa muda mrefu kwa kuwa mtoto anapaswa kuwa jirani na mama ili aweze kuwa na mapenzi na mama yake.
“Ukweli ni kwamba namshukuru sana Mungu kwa kunipa mtoto kwa sababu ni watu wengi wametamani kuwa na watoto kwa hiyo niseme tu kwamba nampenda sana mwanangu na ninajivunia kuitwa mama,” alimsema Linah.
Neema Adrian