
MBUNHGE Viti Maalum Catheline Magige amesimama leo Bungeni kuhoji utaratibu unaotumika kwa ajili kutumia kigezo cha uzoefu jambo ambalo linawanyima nafasi wanafunzi wa Vyuo Vikuu wanaohitimu na kuomba ajira kwenye sekta mbalimbali nchini.
Magige alipohoji suala hilo alijibiwa na Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, William Ole Nasha ambaye amesema kuwa sio kazi zote zinataka uzoefu ikiwa lengo la kuanzisha mfumo wa elimu ambao unafundisha stadi za kazi.