
STAA wa Bongo Fleva, Alikiba jana aliungana na familia, ndugu, jamaa na marafiki kuuaga mwili wa aliyekuwa dansa wake, Emma 4 Real aliyefariki dunia majuzi wakati akipatiwa matibabu hospitalini kutokana na ugonjwa uliokuwa ukimsumbua.
Akizungumza kwa niaba ya madansa wote, Msemaji na Rais wa Chama cha Madansa nchini, Super Nyamwela amesema Alikiba ndiye msanii pekee aliyefika kujumuika nao kuuaga mwili wa marehemu Emma lakini hakuna msanii mwingine aliyejitiokeza, wala kutoa mchango kwa ajili ya msiba huo.
Super Nyamwela amesema madansa wamekuwa wakitumiwa na wasanii au watu wengine kama Big-G, lakini hawathaminiwi, hivyo wameamua kuanzisha chama chao ili kuwaunganisha pamoja na kutetea maslahi yao huku akidai sheria kali zitatungwa ili kukifanya chama hicho kiwe hai. Mwili wa Emma uliagwa jana Dar na kusafirishwa kwenda kwao Chalinze kwa mazishi.