×

PROF JAY Amzungumzia Marehemu Bilago – Video

KUFUATIA kifo cha Mbunge wa Buyungu, wilayani Kakonko, Kigoma (CHADEMA), Kasuku Samson Bilago, mbunge wa Mikumi, Joseph Haule ‘Profesa Jay’ amezungumza na Global TV na kueleza majonzi yake kwa marehemu na atakavyomkumbuka.

 

Bilago alifariki dunia juzi Jumamosi, Mei 26, 2018 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili alipokuwa akipatiwa matibabu.

 

Bilago alizaliwa Februari 2, 1964 na alikuwa mwanachama wa cha Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA). Alichaguliwa kuwa mbunge wa Buyungu kuanzia mwaka 2015 hadi mauti yalipomkuta.