×

Mwili wa Mbunge Bilago Waagwa, Karimjee Dar- VIDEO

MWILI wa aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Buyungu mkoani Kigoma (CHADEMA), Kasuku Bilago aliyefariki dunia juzi Jumamosi, umeagwa Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam kabla ya kusafirishwa kwenda Dodoma kuagwa na wabunge wote.

 

 

Tukio la kuaga limeambatana na ibada fupi ya kuombea mwili wa marehemu iliyofanyika kwa dini ya Kanisa Katoliki viwanjani hapo.

Mamia ya waombolezaji wamejitokeza kuuaga mwili wa marehemu wakiwemo Waziri Mkuu Mstaafu na Mjumbe wa Kamayi Kuu ya Chadema, Edward Ngoyayi Lowassa, Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe, Katibu Mkuu , Vencet Mashinji, Ezekiel Wenje, Godbess Lema na wabunge wengine wa chama hicho wameungana na waombolezaji wengine Katika kutoa heshima zao za mwisho.

Baada ya kuagwa Karimjee, mwili wa Marehemu Bilago utasafirishwa kwenda Dodoma ambapo kesho utaagwa na wabunge wote, bungeni Jijini Dodoma kabla ya kusafirishwa kwenda kwao Kigoma kuzikwa.

Bilago alifariki dunia juzi Jumamosi, Mei 26, 2018 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili alipokuwa akipatiwa matibabu.

KUAGWA KWA MBUNGE BILAGO: Viongozi Watoa Salam za Rambirambi