
MKUTANO Mkuu wa mwaka wa Klabu ya Yanga SC unaendelea muda huu kwenye Bwalo la Maafisa wa Jeshi la Polisi, Oysterbay, Dar es Salaam umefunguliwa na mgeni rasmi, Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Dk. Harrison George Mwakyembe.
Waziri Mwakyembe amewapa miezi miwili Yanga kufanya uchaguzi kujaza nafasi zilizo wazi na amewapa baraka zote kuingia katika mfumo wa hisa.
Mpaka sasa aliyekuwa mwenyekiti wa klabu hiyo, Yussuf Manji hajafika katika mkutano huo licha ya kupelekewa mwaliko wa kuhudhuria mkutano huo.
Wanachama wamefika kwa wingi katika mkutano huo huku baadhi wakiondolewa kwenye mkutano kutokana na sababu mbalimbali.
(HABARI NA WILBERT MOLANDI)