×

MDAU WA MITINDO NA UREMBO AWAKUMBUKA WATOTO YATIMA

Salma akiongea na mmoja wa watoto yatima baada ya kufika kituo cha Abubakar Islamic Foundation.

 

Mdau wa mitindo ya mavazi na urembo, Salma Kader maarufu kama Salma Collection jana aliwatembelea watoto yatima wa Kituo cha Abubakar Islamic Foundation kilichopo Mingoi Bagamoyo na Sifa Foundation kilichopo Vikawe Bagamoyo mkoani Pwani na kubadilishana nao mawazo.

Mmoja wa wasaidizi wakiingiza ndani mizigo baada ya kumpokea Salma.

Salma ambaye alikuwa ameambatana na watoto wake watatu katika ziara hiyo baada ya kubadishana mawazo na watoto hao na kujionea changamoto zinazowakabili aliwakabidhi msaada wa vitu mbalimbali ikiwemo sabuni, mafuta ya kupakaa na kupikia, unga, sukari, maharage, viungo, mchele, ndizi, chokleti.

Akiwagawia baadhi ya vitu alivyowapelekea.

Watoto hao baada ya kubadilishana mawazo na kupewa moyo wa kuwa na mafanikio makubwa katika maisha yao walionesha furaha na kumkaribisha tena siku nyingine wakati akiwaaga.

Sehemu ya zawadi hizo.

Nao walezi wa vituo hivyo walimshukuru Salma kwa kuwakumbuka watoto hao haswa kipindi hiki cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.