×

NEW VIDEO: Kitanda- Foby, Karen & Ibra Nation

Msanii mahiri wa muziki wa kizazi kipya, Frank Ngumbuchi ‘Foby’, baada ya kukaa kimya kwa muda katika gemu, ameibuka upya na kuachia ngoma yake iitwayo Kitanda akiwa amemshirikisha mwanadada Karen na Ibra Nation, ambayo tayari imeshakuwa gumzo mitandaoni kwenye vituo vya redio na runinga.

Foby ambaye yupo chini ya menejimenti ya Nambiza Entertainment, amewashukuru mashabiki wake kwa jinsi walivyompokea kwa mikono miwili, huku akiahidi kufanya mambo makubwa zaidi akiwa na menejimenti yake mpya.

“Yaani hata siamini jinsi nilivyopokelewa vizuri, redioni ngoma yangu inapigwa, kwenye vituo vya runinga na kwenye mitandao ya kijamii ndiyo usiseme, nawashukuru sana mashabiki zangu na wote wanaoniunga mkono, naishukuru menejimenti yangu ya Nambiza Entertainment na nawaomba waendelee kunipa sapoti,” alisema Foby ambaye pia amewahi kutingisha na ngoma yake ya Sio Staa.