×

WATEJA TIGO KUONA KOMBE LA DUNIA LAIVU KUPITIA STAR TIMES APP

Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Matangazo wa Tigo, William Mpinga akizungumza na wanahabari hawapo pichani.

Kampuni ya Simu za mkononi ya Tigo na Star Times jana wamezindua huduma Star Times App ambayo itawawezesha watumiaji wa simu za Smart Phone kujionea kombe la dunia laivu kupitia simu zao.

Mpinga na Meneja Masoko na Matangazo wa Star Times, David Malisa wakitoa ufafanuzi wa huduma hiyo.

Akizungumza na wanahabari kwenye mkutano uliofanyika Hoteli ya Slipway Jijini Dar jana, Mkuu wa Kitengo cha Masoko wa Tigo, William Mpinga alisema katika mchakato huo wao watatoa internet katika kuwezesha mchakato huo na Star Times ndiyo wenye App hiyo.

Wahudumu wa Star Times wakifuatilia kiumakini wakati viongozi hao wakitoa maelekezo kwa wanahabari.

Naye Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Matangazo wa Star Times, David Malisa amewataka watumiaji wa mtandao wa tigo kupakua App hiyo ili kujionea matukio muhimu ya kombe la dunia ambapo watumiaji hao wataweza kurekodi mechi wanayoitaka kwa ajili ya kuitazama vizuri watakapopata muda muafaka.

Mapaparazi wakiwa kazini.
Afisa Uhusiano wa Star Times, Samwel Gisayi akionesha maelekezo ya kupakua App ya Star Times.
Mkuu wa Masoko wa Tigo, William Mpinga (kushoto) na Mkuu wa Masoko na Matangazo wa Star Times, David Malisa wakibadilisha mipira baada ya kumaliza uzinduzi huo.

HABARI/PICHA: RICHARD BUKOS / GPL