The House of Favourite Newspapers

Rihanna Atia Fora Maonyesho ya Mavazi ya ‘Oceans8’

NYOTA wa muziki wa Pop wa Marekani, Rihanna,  jana alitia fora kwenye maonyesho ya mavazi yajulikanayo kama  “Ocean’s 8″  yaliyofanyika Cineworld Leicester Square,   jijini London, Uingereza, ambako alishiriki na mastaa wengine wakiwemo  Sandra Bullock, Cate Blanchett, Anne Hathaway.

Mrembo huyo alikuwa amevaa gauni la rangi ya kijani yenye mng’ao wa dhahabu ambalo liliacha bega moja likiwa wazi na kifuani uwazi wake ukiwa umeshuka zaidi.

Nywele zake zilikuwa zimevutwa kwa nyuma na kukusanywa kwenye kifundo juu ya kichwa, midomo yake ikiwa imeng’arishwa kwa rangi nyekundi na miguu yake murua ikiwa imesimamishwa juu ya viatu vya “mchuchumio” vyenye rangi ya dhahabu nyekundu.

 Msanii Mindy Kaling naye alikuwepo.

Sandra Bullock akipozi kwenye maonyesho hayo.

Sarah Paulson alionyesha ‘manjonjo’ yake pia.

Comments are closed.