The House of Favourite Newspapers

Daktari Ashtakiwa kwa Kuiba Moyo wa Polisi

HII ni hatari sana! Hivi ndivyo unavyoweza kusema baada ya daktari mstaafu nchini Kenya Dkt. Moses Njue ameshtakiwa katika Mahakama ya Meru kwa kosa la kuiba viungo vya maiti za binadamu wakati wa utumishi wake.

 

Mwendesha mashtaka wa kesi hiyo Claire Murithi ameiambia Mahakama kuwa  Dkt. Njue aliiba moyo wa Polisi wa zamani nchini humo, Benedict Karau huku akimtuhumu pia kupoteza ushahidi wa kesi hiyo.

 

Kwa mujibu wa maelezo yaliyotolewa Mahakamani Machi 12, 2015 yalieleza kuwa Dkt. Njue ndiye alikuwa kiongozi mkuu wa uchunguzi wa maiti katika hospitali ya Consolatha, aliiba moyo wa Polisi huyo kabla haujapelekwa katika shule kwa ajili ya kufundishia wanafunzi.

 

Aidha, Dkt. Njue amekana mashtaka hayo huku mahakama ikimtaka kuweka dhamana ya zaidi ya shilingi milioni 45 za kitanzania.

 

Wakili wa Dkt. Njue aliiomba Mahakama kupunguza dhamana hiyo kwa kile alichokidai kuwa mteja wake ni mtumishi wa umma ambapo baadae Mahakama ilimtaka kutoa zaidi ya milioni 11 za kitanzania kama dhamana.

Comments are closed.