×

Ramos Amponda Maradona, Amsifia Messi

Sergio Ramos.

 

BEKI wa Hispania, Sergio Ramos amesema Diego Maradona ameachwa mbali kiuwezo uwanjani na Lionel Messi, pindi unapoamua kuwalinganisha nguli hao wa Argentina.

Diego Maradona

Kauli hiyo ameitoa ikiwa ni kujibu maneno ya Maradona ambaye alinukuliwa akisema kuwa Ramos siyo kiongozi mzuri uwanjani kama ilivyo kwa Diego Godin wa Atletico Madrid.

Lionel Messi.

“Hata Argentina wanajua Maradona ameachwa mbali na Messi, kwangu mchezaji bora kuliko wote kwao ni Lionel Messi,” alisema.