
KITENGO Maalum cha Kufichua Maovu cha Global Publishers (OFM) hivi karibuni kimebaini chimbo ambalo mastaa kibao wa kike Bongo wamekuwa wakitinga kwenda kuchuna mabuzi yao.
Chimbo hilo ambalo ni gesti inayomilikiwa na pedeshee mmoja maarufu jijini Dar lipo maeneo ya Mwananyamala Peace jijini Dar na inadaiwa mastaa wengi hasa wa filamu wamekuwa wakifika eneo hilo wakiwa na mabwana zao hasa nyakati za usiku.
Kisikie chanzo
Awali kijana mmoja aliyedai anaishi jirani na gesti hiyo alipiga simu katika dawati la OFM na kufunguka hivi;
“Jamani hapa Mwananyamala maeneo ya Peace kuna gesti moja inaitwa (anaitaja jina) yaani hapa ni chimbo la mastaa kwa ajili ya kufanyia ufuska wao. Mkija hapa mtabaini mengi,” alisema sosi huyo huku akiomba jina lake lihifadhiwe.
Baada ya ubuyu huyo kuvuja, makamanda wa OFM walitinga eneo hilo na kuweka kambi kwa siku tatu mfululuzo (Ijumaa, Jumamosi na Jumapili kuanzia saa 10 jioni hadi saa sita usiku).
Hata hivyo, ndani ya siku hizo hawakunasa mastaa wenye majina wakiingia eneo hilo, mazingira yaliyomlazimu Kamanda wa OFM kuwasiliana tena na mtoa habari wetu ili kujua kulikoni.
Risasi Jumamosi: Au umetuingiza chaka? Mbona tumeweka mtego pale kwa siku tatu bila kunasa staa yoyote?
Sosi: Siwezi kuwafanyia hivyo, basi tufanye hivi, nikiona staa yoyote anaingia kwenye chimbo hili nitawatonya.
Risasi Jumamosi: Sawa utafanya hivyo, au kama utaweza kupiga picha, itapiga hata kwa simu kisha tutakulipa.
Sosi: Sawa.
Jumanne mchana
Sosi: Haloo..
Risasi: Ee, sema!
Sosi: Hapa namuona yule msanii wa filamu anayeitwa Lungi, anaingia kwenye hii gesti, mnaweza kuja?
Risasi: Sasa, kama unayo simu wewe mpige tu kwa kuibia kisha sisi tutajua la kufanya.
Baada ya mawasiliano hayo, ‘agenti’ huyo wa OFM alifanikiwa kumpiga picha kadhaa staa huyo akitinga kwenye chimbo hilo ambapo inadaiwa alikuwa ameongozana na mwanaume ambaye jina lake halikufahamika mara moja.
Kufuatia picha za msanii huyo kutua kwenye dawati la OFM, mwandishi wetu alifanya jitihada za kumpata ili kujua kilichompeleka katika chimbo hilo, alipopatikana kwenye simu alitoa povu si la nchi hii.
“Acheni kufuatilia mambo ya watu, hamjui naishije, mimi kwenda pale kunawahusu nini?” Alihoji Lungi kabla ya kukata simu na hata alipopigiwa tena hakupokea.
Hata hivyo, OFM bado wapo kazini ili kuwabaini wasanii wengine wanaoenda kwenye chimbo hilo.