SENEGAL wamepambana na kupata pointi moja muhimu katika mchezo dhidi ya Japan kwenye Kombe la Dunia leo nchini Urusi, baada ya sare ya 2-2 dhidi ya Japan.
Senegal, timu yenye kocha pekee rasta katika World Cup mwaka huu, Aliou Cisse ambaye mwaka 2002 akiwa kiungo, aliiongoza timu hiyo hadi robo fainali ya Kombe la Dunia, ndiyo iliyobeba matumaini ya Waafrika wengi. Hii ni michuano ya pili tu kwa Senegal katika Kombe la Dunia.
Afrika imebakiza timu mbili tu katika Kombe la Dunia hadi sasa, Waarabu wote; Morocco, Misri na Tunisia walishayaaga mashindano, wamebaki kukamilisha ratiba tu. Nigeria na Senegal ndiyo timu pekee za Afrika ambazo zina nafasi ya MOSCOW, Urusi kutinga 16 bora.

Matokeo ya jana, yanamaanisha kwamba Senegal na Japan zina pointi nne, zikiwa kileleni mwa Kundi H. Wababe wengine wa kundi hilo, Poland na Colombia walitarajiwa kucheza jana usiku, wote wakiwa hawana pointi yoyote baada ya kuchapwa katika mechi zilizopita.

Poland alichapwa na Senegal 2-1, halafu Colombia akapokea kichapo kama hicho kutoka kwa Japan. Pointi hiyo, imeiweka Senegal katika nafasi nzuri ya kufuzu hatua ya 16 bora, hasa kama inaweza kuambulia angalau sare katika mchezo wa mwisho dhidi ya Colombia Alhamisi.
Katika mchezo wa jana, bao la kwanza la Senegal lilifungwa na Sadio Mane dakika ya 11, lakini Japan walisawazisha kupitia kwa winga wa Real Betis ya Ligi Kuu Hispania (La Liga), Takashi Inui.

Senegal walionekana kuelekea ushindi wakati beki kinda mwenye miaka 19 anayeichezea K.A.S. Eupen ya Ubelgiji, alipofunga bao la kuongoza dakika ya 71, lakini Keisuke Honda anayeichezea C.F. Pachuca ya Mexico akasawazisha dakika ya 78. Senegal inaingia katika mchezo wa mwisho dhidi ya Colombia, Alhamisi ikiwa na matumaini makubwa ya kufuzu.
JAPAN: Kawashima, Hiroki Sakai, Yoshida, Shoji, Nagatomo, Haraguchi (Okazaki 75), Hasebe, Shibasaki, Inui (Usami 87), Kagawa (Honda 72), Osako;
Subs not used: Higashiguchi, Ueda, Endo, Muto, Yamaguchi, Oshima, Makino, Gotoku Sakai, Nakamura
Goals: Inui (34), Honda (78)
Bookings: Inui, Hasebe
Manager: Akira Nishino
SENEGAL: Khadim N’Diaye, Sabaly, Koulibaly, Sane, Wague, Badou Ndiaye ((N’Doye 81), Alfred N’Diaye (Kouyate 64), Gueye, Sarr, Niang (Diouf 85), Mane;
Subs not used: Diallo, Mbengue, Mbodji, Sow, Konate, Sakho, Balde, Gassama, Gomis
Goals: Mane (12), Wague (71)
Bookings: Niang, N’doye
Manager: Aliou Cisse
Referee: Gianluca Rocchi (Italy)