×

KIBAJAJI ‘Ampiga Marufuku Nape’ Kuizungumzia CCM – Video

Mbunge wa Jimbo la Mtera (CCM), Livingstone Lusinde ‘Kibajaji’, akichangia hoja bungeni, amemjibu Mbunge mwenzake wa Mtama, Nape Nnauye (hakumtaja jina) na kumtaka aache kukizungumzia chama hicho ndani ya Bunge na badala yake kama ana hoja zinazohusu chama azipeleke kwenye vikao vya ndani vya chama.

 

Kauli hiyo ya Lusinde imekuja baada ya Nape kudai kuwa, CCM inaenda kufa kwa Kanda ya Kusini kwa madai ya kushindwa kuwajali wakulima wa korosho. Lusinde alidai kuna mbunge ametoa kauli hiyo ya CCM kufa (Nape) huku akitolea mfano kuwa Chadema hawajawahi kusimama bungeni wakaema chama chao kinaelekea kufa.

 

FUATILIA KAULI HIYO HAPA