×

EXCLUSIVE: KAGERE ASAINI MIAKA MIWILI SIMBA

Mchezaji aliyekuwa akiichezea Gor Mahia FC ya Kenya, Meddie Kagere, amesaini mkataba wa miaka miwili kuitumikia klabu ya Simba.

 

Kagere aliwasili jana jijini Dar es Salaam kwa ajili ya mazungumzo na mabingwa hao wapya wa Ligi Kuu Bara msimu wa 2017/18 na kufanikiwa kufikia makubaliano.

 

Mchezaji huyo aliyeng’ara katika mashindano ya SportPesa Super Cup huku akiwafunga Simba moja ya bao kati ya mawili katika mchezo wa fainali, amemalizana na uongozi wa klabu hiyo mpya akiwa chini ya wakala wake, Patrick Gakumba.

 

Kagere ameungana na beki kutoka Ivory Coast, Pascal Wawa ambaye naye imeelezwa tayari ameshamalizana na Simba japo bado haijawekwa wazi kama ameshasaini mkataba.

 

Ujio wa Kagere unaweka wasiwasi nafasi ya Laudit Mavugo kutoka Burundi ambaye hapewi nafasi kubwa ya kuendelea kusalia katika kikosi cha Simba kuelekea msimu ujao wa Ligi Kuu Bara.