×

JPM: Nimechoka Kutuma Rambirambi, Waziri Hashiriki Hata Kuzika? – Video

Rais Dkt. John Magufuli amesema amechoka kutuma salam za rambirambi kufuatia ajali mbalimbali zinazotokea hapa nchinikwa uzembe wa watu wachache kugharimu maisha ya watu huku akimtaka Waziri Mpya wa Wizara ya Mambo ya Ndani, Kangi Lugola kuhakikisha anasimamia jambo hilo kupunguza ajali zinazozuilika.

 

Magufuli ameyasema hayo leo Julai 02, 2018 Ikulu jijini Dar es Salaam baada ya kuwaapisha viongozi aliyowateua jana Jumapili kuziba nafasi za viongozi wengine aliyowaengua na waliostaafu.

 

“Ajali barabarani, nimechoka kutuma rambirambi, unatuma hujamaliza wiki unatuma tena, kinachosikitisha Waziri wa Mambo ya Ndani hatumi hata rambirambi wala hahudhurii kuzika, unasikia tu yuko huko….! hakuna hatua zinazochukuliwa.

 

“Mkoa wa Mbeya katika wiki mbili wamekufa watu 40 kwa ajali, majeruhi zaidi ya 100, hakuna hatua zinazochukuliwa, kwa nini RPC na RTO asijiuzulu? Au hadi wafe wangapi? Mpunguzie hata nyota ili ajue damu za watu zinavyouma.

 

“Jeshi la Zimamoto kuna magari 53, mengine ya mwaka 1987, kuyajua haya mpaka tumepeleleza, wahusika wenye wizara waliopewa dhamana wapo tu wala hawataki kuyajua haya, lakini kwenye sherehe wanahudhuria, ukasimamie haya, Zimamoto wawe na uwezo wa kupambana na haya majanga,” alisema Magufuli.

 

Na Edwin Lindege | Global Publishers.

VIDEO: FUATILIA TUKIO ZIMA HAPA