
MSANII wa kitambo kwenye tasnia ya filamu Halima Yahaya ‘Davina’ amesema kuwa biashara zake zikimuendea vizuri ataachana na kuigiza.
Akizungumza na Amani, Davina alisema kuwa sasa hivi ameanza biashara ya kuuza vitu mbalimbali vya urembo lakini yuko mbioni kuzindua na pafyumu yake.
“Yaani biashara zangu zikikaa vizuri tu huwezi amini mambo ya kuigiza naweka kando kabisa maana hakuna tunachopata kama sura tumeuza sana, kipindi hiki ni cha kutafuta pesa tu,” alisema Davina.
Stori: Mwandishi Wetu, Amani