HATIMAYE mwili wa mtoto wa Msanii wa Bongo Muvi, Rose Alphance ‘Muna Love’ umewasili jioni ya leo ya Julai 06, 2018 katika Uwanja wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam ukitokea nchini Kenya ambapo ndugu, jamaa na marafiki wamejitokeza katika kuupokea ambapo hadi sasa bado taratibu za kuutoa ndani ya uwanja huo zinaendelea.
Mpaka mda huu bado mwili wa mtoto huyo haujachukuliwa uwanjani hapo kutokana na taratibu za vibali kuendelea kufanyika.


PICHA: HILALY DAUDI | GPL