×

YANAYOWEZA KUMFANYA MKE AKATEMBEA NA RAFIKI WA MUMEWE!

Image result for AFRICAN BLACK COUPLES

NI wiki nyingine tulivu kabisa tunakutana tena kupitia safu hii nikiamini umzima bukheri wa afya na unaendelea vyema na majukumu yako ya kila siku kama kawaida.

Mimi namshukuru Muumba wa mbingu na ardhi kwa kuniwezesha kutimiza majukumu yangu ya kila siku likiwemo hili la kuelimishana na kukumbushana juu ya mambo yanayogusa maisha yetu ya kimapenzi.

Mpenzi msomaji wangu, wiki iliyopita nilikuwa na kazi kubwa ya kumshauri rafiki yangu ambaye aliniletea mashitaka ya mke wake kutembea na rafiki yake. Nilipata wakati mgumu sana kwani nilipoongea na mke aliniambia wazi kwamba, amekuwa hapati penzi alilotarajia kutoka kwa rafiki yangu.

Msichana huyo akaenda mbele zaidi na kusema kwamba, yule shemeji yake alionesha kumjali sana kiasi kwamba siku alipomtamkia kwamba anampenda ilimuwia ngumu kukataa. Kuna kitu cha kujifunza hapa kwamba endapo utaishi na mkeo bila kumuaminisha kwamba unampenda kwa dhati, akitokea mtu wa pembeni akaonyesha kuwa kafa kaoza, tarajia kusalitiwa kama siyo kuachwa kwenye mataa.

Unapokuwa umeanzisha uhusiano na mtu, utambue ana watu wengi wanao -mtaka lakini huenda anawakatalia kwa kuwa yuko na wewe, sasa ukionesha kutomjali, hawezi kuendelea kuwa muaminifu kwako. Atachepuka na hata kama ataendelea kuwa na wewe ni kwa kuwa labda hana ujasiri wa kukuacha. Ndiyo maana leo nikaona nikupe sababu ambazo zinaweza kumfanya mkeo akatembea na rafiki yako tena wakati mwingine kwa siri bila wewe kujua.

Image result for HAPPY AFRICAN BLACK COUPLES

WEWE MWENYEWE

Endapo utakuwa umeingia kwenye ndoa, wewe mwenyewe unaweza kutengeneza mazingira ya kusalitiwa. Usipoonesha kumpenda mkeo, kumjali, kuthamini penzi lake kisha rafiki yako akayaonesha hayo kwake, ni rahisi sana kukupiku.

Kwa mfano, andapo una mke lakini hata siku moja hujawahi kumpa zawadi au kumtoa ‘out’, siku shemeji yake (rafiki yako) akiamua kufanya hivyo, mkeo atahisi yeye ni mtu sahihi kwake.

KUJIRAHISI KWAKE

Wapo ambao wanatembea na mashemeji zao kwa sababu tu ya kujirahsi kwao. Kwa mfano unapopendelea kuzungumza mambo ya chumbani na rafiki wa mumeo wako unatarajia nini? Unapomvalia kihasara rafiki wa mumeo lengo linakuwa ni lipi? Mbaya zaidi ni pale utakapokuwa na mashemeji ambao hawabipiwi. Hapa namaanisha wale ambao wakiona dalili ya kupendwa tu, wanaomba chansi.

KUMUAMINI SANA

Haishauriwi kumuamini sana rafiki yako kwani wengine wakipewa uhuru wa kuwa karibu na mashemeji zao, huchukulia kama fursa ya pekee.

Kwa mfano, unapomuamini rafiki yako kiasi cha kumruhusu aende na mkeo baa, klabu au ufukweni ni kujitafutia matatizo. Tunajua kwamba wapo marafiki waaminifu lakini tambua tu kwamba wengi wanapokuwa mazingira hayo ndipo huishia kusaliti na wakati mwingine bila kupenda.

Kwa nini nasema bila kupenda? Chukulia umemruhusu mkeo aende baa na rafiki yako, wamekunywa pombe hadi wamelewa kisha rafiki yako anamchukua mkeo kwenye gari kumrudisha nyumbani. Wengi kwenye mazingira hayo uzalendo unawashinda. Kwa hiyo kama hutaki yakukute ya kusalitiwa, kama una tabia ya kumruhusu mkeo kwenda baa na shemeji yake, acha mara moja.Related image

RAFIKI MNAFIKI

Unaweza kuwa na rafiki lakini kumbe ni mnafiki. Huyu ni yule ambaye mko pamoja lakini anajiapiza kwamba siku moja lazima atakumegea penzi lako. Huyu ndiye tunamuita rafiki mnafiki.

Kutokana na tabia hizo ndiyo maana matukio ya baadhi ya wanaume kuwatongoza wake wa marafiki zao yamekuwa yakiongezeka. Pia wanawake wengi sasa hivi hawaoni hatari kuwatongoza marafiki wa waume zao au wapenzi wa mashoga zao.

TAMAA TU

Endapo utagundua mkeo katembea na rafiki yako, kuna uwezekano ameshawishiwa kwa pesa au mali. Hii ni kwa sababu wapo watu ni dhaifu sana, yaani wao kusaliti wapenzi wao kwa sababu ya pesa, mali au tamaa zao za kimwili siyo kitu kigumu.

Ndiyo maana tunashauriwa kuwa na wapenzi ambao hawana tamaa za kijinga. Katika siku za mwanzo za uhusiano wenu ukigundua uliye naye si mtu wa kuridhika na penzi unalompa, pesa na mali mlizonazo, mapema muonesha mlango wa kutokea kwani itakuwa siyo jambo la ajabu kusikia katembea hata na ndugu au rafiki yako.

Ni hayo tu kwa leo, tukutane tena wiki ijayo kwa mada nyingine.