×

Mrundi Simba Ataja Kinachommaliza Wawa

KAIMU Kocha Mkuu wa Simba, Masoud Djuma, raia wa Burundi, ametaja sababu za beki Muavory Coast, Pascal Serge Wawa kutokuwa na kiwango bora kwamba ni kutokana na kutocheza muda mrefu.

 

Wawa ambaye ametua Simba hivi karibuni kwa kufanyiwa majaribio ya kusajiliwa kikosini hapo, ameonyesha kiwango cha chini katika michuano ya Kombe la Kagame.

Akizungumza na Championi Jumatatu, Djuma amesema kuwa, beki huyo anashindwa kuonyesha kiwango chake kutokana na kutopata muda mwingi wa kucheza.

“Shida yake hakucheza kwa muda mrefu kutokana na kumaliza mkataba wake, ndiyo maana inaleta matatizo kwake ya kutocheza vizuri.

“Naamini muda ukiendelea kusonga mbele anaweza akawa vizuri baada ya kupata muda wa kucheza, tutaona huko mbele. Ni miongoni mwa wachezaji wazuri ambaye ana uelewa wa haraka unapomwambia kitu,” alisema Djuma.

Khadija Mngwai, Dar es Salaam.