The House of Favourite Newspapers

Imevuja! Kumbe Nisha Kaiba Mume wa Mtu!

IKIWA ni takribani siku moja tangu staa wa filamu na muziki Bongo, Salma Jabu ‘Nisha’,  kumuanika mwanamume aliyedai kuwa ni mpenzi wake mpya anayejulikana kama ‘Babu Mzungu’ huku akidai kuchoshwa na wanaomnyang’anya mabwana, kusalitiwa na vibenteni, Global Publishers imemuibua mwanamke anayejiita Felisters James ambaye amedai kuwa Mzungu huyo ni mume wake.

Alichokiandika Nisha.

Kupitia akaunti yake ya Instagram, kuna picha ambazo Felister ambaye pia ni Mtanzania aliziachia mwaka jana akimshukuru Mungu kwa kumpa mme mwema ambaye anadaiwa kuwa ni raia wa Urusi.

Mbali na picha za ‘mumewe’ huyo, Felister ameanika picha akiwa na wakwe zake ‘baba na mama’ wa mwanamme wake na kuwashukuru kwa kumzalia mme mwema ambaye wanapendana kwa dhati.

Dada huyo alienda mbali zaidi na kuachia picha za kimahaba akipigana denda na ‘mumewe’ huyo,  jambo ambalo Nisha naye aliachia video ikimwonyesha akipigana denda hadharani na Mzungu huyo.

Kufuatia kutokea kwa picha hizo, mashabiki wamekuwa wakimwandama Nisha na kumtupia maneno makali wakidai kuwa amekubuhu kuiba mabwana za watu na sasa inatosha.

Hata hivyo, bado haijathibitika iwapo Mzungu huyo ni mme wa ndoa wa Felister, iwapo bado wako pamoja au walishaachana.

Global Publishers tunaendelea kufuatilia undani wa sakata hili la Nisha kudaiwa kuiba Mzungu wa watu na kumfanya ‘baby’ wake huku akimwanika bila woga wala aibu mitandaoni.

Endelea kufuatilia Global TV Online, ‘soon’ utaupata ukweli wa jambo hili.

Comments are closed.