×

Cardi B Ajifungua Mtoto wa Kike Aitwaye Kulture Kiari Cephus

MWANAMUZIKI wa rap, Cardi B  wa Marekani juzi (Jumanne) alijifungua mtoto wa kike katika hospitali moja huko Atlanta na kumpa jina la Kulture Kiari Cephus, Jina hilo ni la baba wa mtoto huyo rapa aitwaye  Offset,  ambaye jina lake halisi ni  Kiari Cephus, ambaye alikuwa kando yake wakati wote wa uzazi.

 

Huyu ni mtoto wa kwanza wa Card B na wa wanne kwa Offest, ambapo wawili hao wanaosemekana walioana kwa siri Septemba mwaka jana, wamepanga kuangusha bonge pati ya ndoa baadaye mwaka huu.