×

CHADEMA: CCM Wanavuruga, TAIFA Litakatika, Hakuna UCHAGUZI – Video

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimelalamikia kuwepo kwa barua ya kugushi inayoashiria kuvuruga uchaguzi mdogo unaotarajiwa kufanyika august 12 mwaka huu katika Jimbo la Buyungu na Kata zingine 79 nchi nzima.

 

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam,  Katibu Mkuu wa Chadema, Vicent Mashinji amesema kuwa kumekuwepo na barua ya kugushi iliyofikishwa kwa Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) ambayo inakinzana na barua halisi iliyoandikwa na chama hicho kwenda NEC.

 

Aidha, Dkt. Mashinji amesema, CHADEMA hakina imani na makamishna walioteuliwa hivi Karibuni na Rais Magufuli kwani wengi wao ni makada wa Chama Cha Mapinduzi.

 

Hivi karibuni Tume ya Taifa ya Uchaguzi imetangaza chagzi ndogo za Madiwani katika kata 79 na Ubunge katika Jimbo la Buyungu Mkoani Kigoma.