Meghan na baba yake, Thomas Markle, kabla hajaolewa na mwanamfalme wa Uingereza, Prince Harry.
SAMANTHA ambaye ni dada wa kambo wa Meghan, mke wa mwanamfalme wa Uingereza, Prince Harry, amemtaka Meghan kukumbuka kuwasiliana na baba yao Thomas Markle (53) ili kuendeleza uhusiano wao.
Hii ni baada ya mzee huyo kuwasiliana na bintiye kwenye mtandao wa Twitter akimsihi amtembelee baada ya kwenda kushiriki sherehe za kumbukumbu ya mwaka wa 100 tangu kuzaliwa kwa aliyekuwa rais wa Afrika Kusini, Nelson Mandela.