The House of Favourite Newspapers

Real Madrid Wao Ni Mbappe Tu

Kylian Mbappe.

JINA la Kylian Mbappe linaen­delea kutajwa kuwa mmoja wa wachezaji wanaow aniwa kwa uka­ribu na wababe wa Ulaya, Real Madrid licha ya mche­zaji huyo kusisi­tiza kuwa hana mpango wa ku­hama kutoka Paris Saint-Ger­main (PSG) kwa sasa.

 

Mbappe al­ionyesha kiwango cha juu akiwa na Ufaransa ka­tika Kombe la Dunia na kui­wezesha timu hiyo kubeba ubingwa, ame­kuwa akipigi­wa debe kwa kiasi kikubwa k u s a j i l i w a na kuoneka­na anafaa kuibeba Ma­drid baada ya kuondoka kwa Ronaldo.

 

Tangu Kuondoka kwa Cristiano Ronaldo kwenda Juventus, Madrid au Los Blancos wamekuwa wakipambana sokoni kuhakikisha wanafanya usajili wa staa mkubwa kama ili­vyo kawaida yao kwa ajili ya kuziba pengo hilo.

 

Taarifa za ndani ya Madrid zi­naeleza kuwa Mbappe ambaye ana umri wa miaka 19 bado anaoneka­na kuwa ni chaguo sahihi na ndiyo maana mabosi wanahaha kuhak­ikisha wanalifanikisha hilo.

Sifa zimekuwa nyingi ambazo zi­nambeba chipukizi huyo kusajiliwa ikiwemo kuonyesha makali akiwa na umri mdogo kuanzia ngazi ya klabu hadi timu ya taifa.

 

Kingine ni uwezo wake wa kufun­ga, amekuwa akionyesha makali katika ufungaji licha ya kuwa siyo straika halisi, kazi yake imekuwa nzuri licha ya kuwa amekuwa kati­ka kikosi kimoja na mastraika halisi wenye uwezo wa juu.

 

Hiyo inanogesha kwa kuwa in­aonekana kama anafuata nyayo za Ronaldo ambaye naye alikuwa winga lakini mwenye uwezo mkubwa wa kufunga.

 

Kibiashara pia nyota huyo anaonekana kuwa vizuri kwa kuwa hadi sasa sura yake imekuwa na soko kubwa PSG, hivyo upande mwingine Madrid wanaamini bi­ashara itakuwepo wakimsajili.

Comments are closed.