Na Edwin Lindege | Global Publishers
WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, amesema alilivunja Baraza la Usalama Barabarani kutokana na baraza hilo kukosa tija katika kudhibiti ajali hizo na kwamba atatangaza baraza jipya mwisho wa mwezi huu.
Lugola wameyasema hayo leo Ijumaa akizungumza na wanahabari ofisini kwake, jijini Dar es Salaam aliposisitiza pia kwamba wamiliki wa magari mabovu yanayosababisha ajali watakamatwa na kufikishwa mahakamani,
Pamoja na kutoa onyo kwa askari wanaokula rushwa, kushirikiana na majambazi na kuwabambikizia makosa wananchi, amewataka pia wakimbizi kutoka Burundi kurejea nchini kwao akisema hali ya huko ni shwari.
Alizungumzia pia suala la uwezekano wa mabasi kusafiri wakati wa usiku ambapo alisema atazungumza na wadau wa usafiri kuhusu jambo hilo.
“Julai 31 nitakutana na wadau wa usafirishaji kuzungumza nao ili wanipe mtazamo wao juu ya jambo hili la kutembea usiku,” alisema.
Comments are closed.