×

G Nako: Siwezi Kuua Muziki Wangu

MKALI kwenye gemu la Muziki wa Hip Hop Bongo, George Sixtus Mdemu ‘G Nako’ amefunguka kwamba madai ya mashabiki zake kwamba anaua muziki wake, kutokana na kutoa ngoma mfululizo hayana mashiko.

 

Malalamiko ya mashabiki wa G Nako kwamba anaua muziki wake, yaliibuka baada ya kutoa Wimbo wa Nyatu Nyatu na kutangaza kuachia wimbo mwingine ndani ya siku chache na Bill Nas, na mashabiki kudai hawapi nafasi mashabiki wa kazi zake kufurahia ngoma bali anawalimbikizia.

 

Akipiga stori na Over Ze Wikiend, G Nako alisema kwamba; “Wimbo ukishafika mtaani umefika. Hata ukitoa nyimbo kumi mfululizo mashabiki wana uwezo wa kusikiliza zote.

“Zaidi ni fursa kwako kama msanii kwani unaweza kuandaa hata shoo ya peke yako bila kutegemea kuwa na kundi lingine la wasanii.”

BONIPHACE NGUMIJE