
RAPA chipukizi wa Bongo, Harmorapa amefungukia kuhusu mahaba yake ya kupitiliza na kaumua kuchora tattoo ya jina la Malkia wa Bongo Movies, Wema Sepetu shingoni kwake ambapo ameanika jinsi anavyomzimia mwanadada huyo.

Harmorapa ameamua kufanya hivyo ikiwa ni siku chache baada ya mwanadada kutoka Mwanza anayedaiwa kuwa ni mpenzi wake mpya, Madam Ziot kuchora tattoo ya Harmorapa begani mwake akionyesha mahaba kwa mpenzi wake huyo.
Harmorapa amefunguka na kudai hana mpango wa kumuoa mwanamke aliyetoka Mwanza kwa ajili yake aliyejitambulisha kwa jina la Khadijah na kudai anataka kumuoa Wema.