×

Miss Kanda Ya Kaskazini Kuisimamisha Arusha

KESHO Jumamosi, warembo 12 kutoka mikoa ya Arusha na Kilimanjaro, wanatarajiwa kusimamisha shughuli za Mkoa wa Arusha pale watakapopanda jukwaani kuwania Taji la Miss Kanda ya Kaskazini 2018 katika Ukumbi wa Hoteli ya Naura Spring jijini hapa.

 

Mkurugenzi wa Kampuni ya Kismaty Advert Media Company Ltd ambayo ndiyo imeandaa shindano hilo, Mary Mollel, amesema washiriki watatu kati ya hao 12, wataungana na wengine kutoka mikoa mingine kuwania Taji la Miss Tanzania 2018.

 

Naye Ofisa Michezo na Utamaduni wa Jiji la Arusha, Benson Maneno, alisema wamesitisha kutoa vibali vyote vya burudani ili kuwapa nafasi wakazi wa jiji hilo kushuhudia shindano hilo ambapo ile shoo ya Juma Jux na Vanessa Mdee iliyopangwa kufanyika kesho Jumamosi katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, imeahirishwa.

 

Shindano la Miss Kanda ya Kaskazini, litasindikizwa na burudani ya muziki kutoka kwa msanii wa Bongo Fleva, Faustina Charles ‘Nandy’ ambapo kiingilio VIP A ni Sh 50,000, VIP B Sh 20,000 na viti vya kawaida Sh 10,000.

Stori na Kennedy Lucas, Championi Ijumaa