×

Ibada ya Kuaga Mwili wa Mama wa Shigongo Kanisani (Picha + Video)

 

 Mwili wa marehemu Bi. Asteria Kahabi Kapela ukiingia katika Parokia ya Mt. Agata, Mikocheni B kwa ajili ya kufanyiwa misa leo.
Wajukuu wa marehemu wakiwa wamebeba jeneza la mwili wa bibi yao.
Mkurugenzi Mtendaji wa makampuni ya Global Group, Eric James Shigongo (kushoto), akiangalia jeneza lilobeba mwili wa mama yake.
Waombolezaji na wanafamilia wakiwa kanisani.
Padri akiendesha misa.
Jeneza lilobeba mwili wa marehemu.
Baadhi ya wajukuu wa marehemu.

IBADA maalum ya kuombea mwili wa marehemu Bi. Asteria Kahabi Kapela aliyefariki dunia juzi Ijumaa, Julai 27, 2018 katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete, Muhimbili jijini Dar es Salaam imefanyika leo katika Kanisa Katoliki la Mikocheni B, Parokia ya Mt. Agata.