MAZISHI ya mama wa Mkurugenzi Mtendaji wa Makampuni ya Global Group, Eric Shigongo, marehemu Asteria Kapela, yamefanyika jana Agosti 1, 2018 katika kijiji cha Bupandwamhela Wilayani Sengerema yakihudhuriwa na maelfu ya wakazi wa maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Mwanza.
Katika usia wake, Shigongo amesema kuwa hakika ni pigo kwake na kwa familia kwa ujumla kwani ameondokewa na mtu muhimu katika maisha yake na Mwenyezi Mungu ampumzishe katika nyumba yake ya milele daima kwani atamkumbuka siku zote za maisha yake na ataendelea kutenda yale yote aliyojifunza kutoka kwake.

Katika mazishi hayo viongozi mbalimbali wa vyama na serikali wamejitokeza kuungana na familia hiyo katika msiba huo, ambao ni pamoja na Waziri wa Kilimo na Mbunge wa Buchosa (CCM) Dkt. Charles Tizeba, mbunge wa zamani wa Nyamagana na aliyekuwa waziri wa zamani wa mambo ya ndani, Lawrence Marsha.
Pia miongoni mwao ni Mbunge wa Mtama (CCM) Nape Nauye, na mchekeshaji Masanja ‘Mkandamizaji’.









