MSANII Lulu Abass ‘Lulu Diva’ ambaye kwa sasa anakimbiza kwenye gemu la Bongo Fleva na Wimbo wa Ona ambao amemshirikisha Rich Mavoko, usiku wa kuamkia leo amefanya tukio la aina yake baada ya kumwaga pesa kibao kwenye ndoa ya mwanasoka Abdi Banda, na dada mdogo wa msanii wa Bongo Fleva, Alikiba, anayeitwa Zabibu Kiba, jijini Tanga.