The House of Favourite Newspapers

NMB YATOA MAFUNZO KWA VYAMA VYA USHIRIKA VYA WAKULIMA SIMIYU

Benki ya NMB  imetoa mafunzo kwa zaidi  ya Vyama Vya Msingi 1, 000 Vya Ushirika wa Wakulima (AMCOS) ya kilimo na utunzaji fedha ndani ya Mwaka mmoja yenye lengo la kuboresha sekta ya kilimo nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari jana  katika madhimiso  ya kilele cha siku ya wakulima  nchini ( Nane nane ) Mkoani Simiyu, Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya NMB, Ineke Bussemaker  alisema benki yake imeamua kusaidia kuboresha sekta ya kiliomo kutokana na umuhimu wake katika kuchangia ukuaji wa uchumi wa nchi na pia kuboresha uchumi wa wakulima.

 

Alisema kuwa mafunzo hayo ambayo bado yanaendelea  sehemu mbali mbaloi nchini yanatarajiwa kuwafikia wakulima wengi  zaidi kupitia vyama vya ushirika na hivyo vitawezesha kuboresha kilimo na kuleta mabadiliko ya kiuchumi katika ngazi ya jamii na nchi kwa ujumla.

Alisema kuwa sekta ya kilimo ni uti wa mgongo wa uchumi wa nchi na kuajiri watanzania zaidi ya asilimia 70, hivyo inapaswa kuboreshwa ili kutoa mchango mkubwa katika maendeleo ya kiuchumi.

 

 

Bi. Bussemaker alisisitiza kuwa unatakiwa ushirikiano wa wadau mbalimbali wa mendeleo ili kusaidia sekta ya kilimo kukua kwa haraka na kuleta tija kwa wakulima na nchi kwa ujumla na kuwa ikiachiwa serikali peke yake  haitaweza kuleta mabadiriko hayo kwa haraka.

Alisema kuwa benki yake inaamini kuwa sekta ya kilimo inao uwezo mkubwa wa   kuleta mapinduzi ya kweli katika uchumi endapo kilimo kitaboreshwa nchini na kwamba sekta hiyo itakuwa na mchango mkubwa katika kufikia malengo ya serikali ya uchumi wa viwanda.

 

 

Bi. Bussemaker alisema kuwa  mbali na mafunzo hayo benki yake imekwisha tumia zaidi ya shilingi bilioni 100 katika kuboresha sekta ya kilimo nchini kwa kutoa mikopo mbalimbali pamoja na huduma zingine za kifedha kwa wakulima nchini.

 

 

“ Ndani ya miaka michache ijayo, tunatarajia kutumia kiasi cha shilingi bilioni  500 katika sekta kuwezesha shughuli za kilimo katika mnyororo mzima wa thamani, hivyo nawaomba wakulima kutokukata tamaa na kilimo kwani benki  yao ipo pamoja nao katika kuhakikisha inaleta mageuzi ya kilimo kwa manufaa na maendeleo ya wakulima na nchi kwa ujumla” alisema Bi. Bussemaker.

 

 

Bussemaker aliwataka wakulima kutumia NMB Bank katika kuleta mageuzi chanya katika kilimo na kuinua uchumi wa Tanzania kufikia uchumi wa kati kwa kuzalisha malighafi zaidi ndani ya nchi ambazo zitatumika katika  viwanda vilivyopo nchini kwa kuwa mkulima akilima zaidi viwanda vinapata malighafi zaidi.

 

 

Comments are closed.