
Dada wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Monica Joseph Magufuli amefariki dunia asubuhi leo Agosti 19, 2018 katika Hospitali ya Bugando jijini Mwanza alikokuwa akipatiwa matibabu.
Rais Magufuli jana alifika katika chumba cha wagonjwa mahututi (ICU) katika Hospitali ya Bugando jijini Mwanza kumjulia hali.

NASIKITIKA kuwajulisha kuwa Dada wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Bi. Monica Joseph Magufuli amefariki dunia asubuhi leo tarehe 19 Agosti, 2018 katika hospitali ya Bugando Jijini Mwanza. Natoa pole kwa Mhe. Rais Dkt. J.P Magufuli, Familia na wote walioguswa na msiba huu pic.twitter.com/q5FwQk3kdj
— Gerson Msigwa (@MsigwaGerson) August 19, 2018