MSANII wa muziki wa kizazi kipya, Juma Mussa ‘Jux’, ametamka kuwa kwa sasa anaweka pembeni ziara yake na msanii mwenzake, Vanessa Mdee ‘V Money’ ya In Love With Money kisha kuelekeza nguvu katika kutengeneza video na nyimbo.
Jux amekuwa akifanya ‘tour’ hiyo ya In Love With Money pamoja na V Money ambaye pia ni mpenzi wake ambapo wawili hao wamezunguka mikoa mbalimbali kwa ajili ya tour hiyo.
Akizungumza na Kilinge, Jux anayetamba na ngoma kibao zikiwemo Looking For You, amesema kwa sasa anadili zaidi na kutengeneza nyimbo zake yeye kama yeye na kuweka pembeni kwa muda suala la tour yao hiyo.
“Kwa sasa ninataka kuja na projekti zangu mimi kama mimi na siyo tena na Vanessa kama ambavyo tumekuwa tukifanya kwenye hii tour ya In Love With Money, ninachofanya ni kutengeneza video na nyimbo zangu.
“Unajua hiyo tour haijafika mwisho, tutaendelea kuifanya ila kwa sasa ninafanya mambo yangu kama mimi kisha baadaye tena tutarudia kuzunguka mikoa mbalimbali,” alisem a Jux.
Said Ally, Dar es Salaam.