The House of Favourite Newspapers

Okwi Hatihati Kuwavaa Wajeda Leo

Emmanuel Okwi

STRAIKA matata na mfun­gaji bora wa Ligi Kuu Bara msimu uliopita, Emmanuel Okwi ana asilimia 75 za kuanza kwenye pambano la leo dhidi ya Tanzania Prisons kwenye mchezo wa ufunguzi wa ligi msimu wa 2018/19.

 

Mshambuliaji huyo amekuwa kwenye hati­hati hiyo baada ya kupa­ta maumivu ya mgongo kwenye mchezo wao wa Ngao ya Jamii dhidi ya Mtibwa, Jumamosi iliyo­pita. Katika mchezo huo Simba walishinda kwa mabao 2-1.

 

Akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari jana, Mkuu wa Kitengo cha Habari cha Simba, Haji Manara amesema jopo la madak­tari wa timu hiyo wanaende­lea kumpa matibabu straika wao huyo kiwembe kuhak­ikisha anakuwa sehemu ya kikosi kitakachoanza katika mchezo huo.

 

“Hadi sasa katika timu hakuna majeruhi yeyote isipokuwa Emmanuel Okwi ambaye ana asilimia 75 za kucheza pambano letu hili mbele ya Tanzania Prisons,” alisema Manara.

 

Katika hatua nyingine, mkuu huyo wa habari aliongeza kwamba mch­ezo huo utapigwa saa moja usiku huku viin­gilio vitakuwa elfu tatu kwa mzunguko, elfu 10 kwa watakaokaa VIP B na ile A ni elfu 15, pia elfu moja mia tano (1,500) maalum kwa watoto,” alisema Manara.

Waandishi: Gray Paul, Adrian Mayunga na Said Ally.

Comments are closed.