×

Yanga Kumenoga, Yawapiga Mtibwa 2-1, Makambo Atupia (Video+ Picha)

Kikosi cha timu ya Yanga SC.

RUDI Yanga kumenoga! Ndivyo unaweza kusema baada ya Yanga, jana kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Mtibwa Sugar katika mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Yanga ambayo miezi ya hivi karibuni ilikuwa kwenye hali mbaya jambo ambalo mashabiki wengi wa timu hiyo walianza kukata tamaa huku wengine wakiikacha, hivi sasa wanapaswa kurudi kuendelea kuzifaidi raha zinazojiri kila siku kikosini hapo.

Kikosi cha timu ya Mtibwa.

Katika mchezo huo wa jana, Yanga ilicheza soka  la kuvutia licha ya kukum­bana na ushindani mkubwa kutoka kwa Mtibwa Sugar.

Mabao ya Yanga yalifun­gwa na Heritier Makambo dakika ya 31 akiunganishwa kwa kichwa krosi ya Gadiel Michael, huku Kelvin Yon­dani akipigilia msumari wa mwisho dakika ya 40 kwa mkwaju wa penalti baada ya Mrisho Ngassa kuchezewa madhambi eneo la hatari na Issa Rashid ‘Baba Ubaya’.

Mpaka kipindi cha kwanza kinamalizika, Yanga ilikuwa ikiongoza kwa mabao hayo.

Ndani ya kipindi hicho cha kwanza, kiungo matata wa Yanga, Feisal Salum ‘Fei Toto’, alifanikiwa kucheza kwa umakini na ustadi mkubwa kwani alikimaliza kwa kupiga jumla ya pasi 22 na zote ziliwafikia walengwa.

 

Kipindi cha pili, timu zote zilikuwa zikisham­buliana kwa kush­tukiza ambapo dakika ya 72, Mtibwa walijipa­tia bao moja kupitia kwa Haruna Chanongo na mpaka mwa­muzi kutoka Singida, Meshack Sud ana­puliza filimbi ya mwisho, Yanga iliibuka na ushindi wa mabao 2-1.

 

Kwa ushindi huo Yanga sasa ina pointi tatu sawa na Simba, zote zikiwa zimeu­tumia vema uwanja wa nyumbani.

 

Kwa takwimu hizo ni dalili nzuri kazi ya kuwania ubingwa imeanza mapema kwa timu hizo za Dar kushindana, Simba ikiw ani bingwa mtetezi wakati Yanga inataka kurejesha makali baada ya kuy­umba msimu uliopita.

 

Matokeo ya mechi zingine za jana kab­la ya usiku Azam haijacheza na Mbeya City yalikuwa hivi; JKT Tanzania 0-0 KMC na Stand United 1-0 African Lyon.

(PICHA: RICHARD BUKOS NA MUSA MATEJA | GPL)