×

NDOA YA JIMMY MAFUFU NA MKEWE ILIVYONOGA KANISANI

Mafufu akimvisha pete mkewe.

Msanii wa filamu za Kibongo, Jimmy Mafufu leo amefunga pingu za maisha na aliyekuwa mpenzi wake Upendo Meja katika Kanisa la AKUZAMU lililopo Kinondoni Biafra Jijini Dar.

 

Katika ndoa hiyo vifijo na nderemo vililindioma kanisani hapo haswa wakati wawili hao wakilishana viapo na baada ya kutangazwa kuwa wawili hao ni mke na mume.

Wakiwekewa mikono mikono ya baraka.

Ndoa hiyo ilionekana kuwa ya furaha kufuatia maharusi hao wageni waalikwa pamoja na waumini wa kanisa hilo kuserebuka sebene la nguvu lililokuwa likiporomoshwa na bendi ya kanisa hilo.

Mafufu akiwawekea mkewe mazingira mazuri ya mahali alipoketi.
Wakionesha vyeti vyao.
Wakicheza sebene baada ya ndoa.
Maharusi wakiwa full furaha.

PICHA NA RICHARD BUKOS | GPL