The House of Favourite Newspapers

Breaking News: Abdul Nondo Akutwa na Kesi ya Kujibu

Mahakama ya Mkoa wa Iringa imemkutwa na kesi ya kujibu Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanafunzi (TSNP), Abdul Nondo anayekabiliwa na mashtaka ya kusambaza taarifa za uongo akidai kutekwa, leo Jumatatu Agosti 27.
Akitoa uamuzi huo baada ya kupitia upande wa mashtaka, Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Mkoa wa Iringa,  Liad Chamshama amesema kutokana na uamuzi huo, Nondo anatakiwa kujitetea dhidi ya mashtaka yanayomkabili ambapo anatarajia kuleta mahakamani mashahidi wasiopungua watano kutoa ushahidi katika kesi yake hiyo ambayo imepangwa kusikilizwa kati ya Septemba 18 na 19, mwaka huu.
Nondo ambaye pia alikuwa mwanafunzi wa mwaka wa tatu katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), kabla hajasimamishwa masomo kutokana na kesi hiyo, anadaiwa kusambaza taarifa za uongo akiwa jijini Dar kuwa ametekwa na shtaka la pili anadaiwa kutoa taarifa za uongo kwa polisi katika Kituo cha Mafinga mjini Iringa.

MPAKA HOME: Maisha Halisi ya Jike Shupa / Amtolea Povu Shilole

Comments are closed.